asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Thursday, May 11, 2017

HAJI MANARA KUMBURUZA KORTINI, SHABIKI WA YANGA ALIYESAMBAZA TAARIFA ZA UONGO FACEBOOK ZILIZOHUSU BASI LA SIMBA KUPATA AJALI KWA HOJA HIZI ZENYE UZITO WA AINA YAKE


Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Sunday Manara ameiomba mamamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, imchukulie hatua shabiki wa Young Africans, Pascal Lameck aliyeposti kwenye mtandao wa kijamii wa facebook taarifa ya uongo kuwa basi la wachezaji wa Simba limepata ajali na wachezaji wote wamevunjika mguu, huku kocha wao, Joseph Omog akiwa hajulikani alipo.

Kupitia posti aliyoitoa kwenye mtandao wa facebook, Manara amehoji uhalali wa shabiki huyo kuendelea kuwepo uraiani akitazamwa bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria na mamlaka ya mawasiliano ya TCRA.

“Always huwa najiuliza mashabiki wa aina hii tunawaacha kwa nini?  Na TCRA ichukue hatua, tusingoje hadi watukanwe wakubwa tu, hatuwezi kusamehe kila kitu,” ameandika Manara kwenye posti yake aliyoiambatanisha na posti ya shabiki huyo.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt