asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Sunday, May 7, 2017

KUMEKUCHAA...!!!! HATIMAYE CHANZO CHA AJALI ILIYOUA WANAFUNZI ZAIDI YA 30 WA SHULE YA LUCKY VICENT CHAJULIKANA....HIKI HAPA....

Wakuu,
Kabla ya yote, natoa pole kwa familia, Ndugu na marafiki waliofikwa na msiba huu katika ajari ya Bus.

Lakini pia nitoe pongezi kwa watanzania wenzangu ambao kwa namna moja au nyingine wameshiki katika kuwatia moyo na kuwapa pole wafiwa.

Ni kweli tujuavyo kwamba ajari haiepukiki lakini kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia kuna baadhi ya ajari zinaepukika.

Kwa utafiti mdogo niliyo ufanya nimegundua baadhi ya mambo ambayo yamepelekea kutokea kwa vifo vingi vya wanafunzi hawa.

1. SEAT BELT
Kuna kila dalili Bus haikuwa na seat belts, na hata kama ilikuwepo wanafunzi hawakufunga ile mikanda. Ukiangalia mwonekano wa Bus, sehemu kubwa iliyopondeka ni sehemu ya Mbele na karibia robotatu ya Bus halijapondeka Sana. Sasa kama kila mwanafunzi angekuwa kafunga mkanda wanafunzi waliokaa siti za nyuma wengi wangepona.

Kwa sababu hakukuwa na seat belt ilipelekea wanafunzi na walimu wao wote kulushwa mbele ya gari baada ya gari kukita kwenye kolongo.

2.UZEMBE WA DEREVA
Kuna kila dalili palikuwa na uzembe. Dereva alikuwa speed kubwa na gari likamshinda kwenye kona ukizingatia na ubichi wa barabara kutokana na mvua zinazoendelea.

OMBI LANGU:
wazazi/Waalimu tuwe makini muda wote na hawa watoto wetu hasa kwenye hizi School Bus, kuna ka tabia ka kulundika watoto, unakuta seat ya watu wawili watoto wamewekwa wanne. Inapelekea watoto kushindwa kufunga mikanda.

Mungu atusaidie!

By The Tomorrow People/JF


2 comments:

  1. Kazi yake mola haina makosa. R.I.P wadogo zangu

    ReplyDelete
  2. Nakuunga mkono kwaasilimia nyingi juu ya ufafanuzi wa ajali hii yakusikitisha,je unafikiri wantanzania wote kwaujumla wanaweza kuhamasishwa vipi ilikuweza kufuata vipengele vya usalama wa barabarani? Naomba nitoe mfano mmoja tu mwepesi, tumekua tukiwaona watanzania wengi tu mara kwa mara kwenye magari yawazi kama pickup za mizigo ambazo hazina hata maali pakujishikilia( vitu kama ivi ingekua vizuri kama sheria ingeweza kufuatilia vizuri kuliko kusubiri paka ajali itokee then ndio tuanze kukemea. "AJILI HUEPUKIKA"

    ReplyDelete

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt