asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Wednesday, June 28, 2017

BREAKING NEWS: JAMAL MALINZI NA MWESIGWA WAMESHIKILIWA NA POLISI.... TAZAMA HAPA SAKATA ZIMA LILIVYOKUWA


Related image
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania, (Takukuru) imethibitisha kumshikilia Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na katibu wake, Mwesigwa Silentine kwa mahojiano ambayo hakuyaweka wazi

Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Mussa Misalaba amethibisha kuwa viongozi hao walikamatwa kwa ajili ya uchunguzi ambapo amesema kuwa Jamal Malinzi na wengine wanaendelea kuhojiwa kwa tuhuma mbalimbali.

Kuhusu ufafanuzi wa tuhuma hizo, ofisa huyo alikataa kuzitaja kwamba ni suala la kiuchunguzi.

Pia alipoulizwa sasa ni lini viongozi hao watafikishwa mahakamani alisema hawezi kusema kwani inawezekana kama watuhumiwa hao wakitoa ushirikiano kwa Takukuru wa ushahidi wanaweza wasifikishwe mahakamani.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt