asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Saturday, June 17, 2017

MBEYA CITY HAWATAKI MCHEZO, WAKAA MEZANI NA SAMATTA BAADA YA KUDAI YEYE NI MCHEZAJI HURU,,. TAZAMA HAPA WALICHOKIZUNGUMZA ILI KUMSAJILI

Image result for KOCHA WA MBEYA CITY
Mbeya City inamuwinda mshambuliaji wa Prisons, Mohamed Samatta katika kuimarisha kikosi chake kwa msimu ujao.

Samatta tayari imefanya mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya na Prisons ingawa mwenyewe amesema mazungumzo hayo hayamzuii kupokea ofa nyingine.

Kocha wa Mbeya City, Mmalawi Kinnah Phiri alipendekeza usajili wa Samatta ambapo alisema kuwa mchezaji huyo atasaidia kuziba pengo la Kenny Ally aliyesajiliwa na Singida United kwa madai ya kwamba uwezo wao kisoka unafanana.

Samatta msimu uliopita ameifungia Prisons mabao matano katika Ligi Kuu Bara.

Samatta alisema mkataba wake na Prisons ulikuwa wa mwaka mmoja, amefanya mazungumzo na viongozi ambapo anaamini kwamba watafikia muafaka na anafurahia maisha ya hapo kwa kipindi chote alichoishi na Prisons.

"Kuhusu Mbeya City pengine wao wameniweka kwenye mipango yao ila bado hawajaniambia jambo lolote, nimemaliza mkataba na Prisons tumezungumza ila bado hatua ya mwisho hivyo sizuiliwi kupokea ofa kutoka timu nyingine kwani mimi ni mchezaji huru."


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt