Balozi huyo mwenye miaka 62, alipigwa risasi kadhaa na mtu huyo aliyekuwa amesimama nyuma yake huku akipiga kelele, Allahu Akbar, We die in Aleppo, you die here!’ Alisikika akisema pia, ‘Only death will take me out of here.’
Muuaji huyo aliyekuwa amevaa suti na tai, amejulikana kwa jina la Mevlüt Mert Altintas, 22. Alidai kupiga kwanza risasi hewani kabla ya kumlenga balozi huyo.
Baada ya hapo aliwageukia watu wengine waliokuwa hapo na kuwajeruhi watatu kabla ya naye kuuawa na polisi.
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amelaani vikali tukio hilo.
Mauaji hayo yamekuja baada ya siku kadhaa za maandamano nchini Uturuki dhidi ya namba Urusi inavyohusika nchini Syria.
No comments:
Post a Comment