SLIDE MANENO
Saturday, December 10, 2016
CLINTON AMIMINA LAWAMA KWA INTERNET
Aliyekuwa mgombea wa Urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Hillary Clinton, ameonya kuhusu ‘vitisho hatarishi vya habari na propaganda za uongo zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii katika kipindi cha mwaka huu.
Alisema kuwa habari hizo za uongo zina madhara makubwa katika ulimwengu wa kweli yakiwemo maisha ya watu wa kawaida. Amedai kuwa ni vitu vya hatari la muhimu kushughulikiwa mapema.
Wakati wa kampeni, Clinton alikuwa shabaha kubwa zaidi ya tovuti za habari za uongo kwenye mtandao wa Facebook ukilinganisha na mpinzani wake, Donald Trump. Kambi yake imekuwa ikidai kuwa habari hizo zimechangia kwa kiasi kikubwa kumkosesha Urais.
Akizungumza Alhamis hii nchini humo, Clinton ameeleza kuwa kuenea kwa habari hizo ni tishio kwa demokrasia
Labels:
HABARI KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment