Wakizungumza kijijini Olgilayi wanawake waliopatwa na mkasa wa kusulubiwa na watu hao wanasema wamekua wakilazimishwa kufanya vitendo vya ngono na pale wanapokataa hupewa adhabu ya kipigo.
Matukio hayo yamewalazimu baadhi ya wazee na vijana kukutana na kuiomba serikali kuchukua hatua za haraka kukabiliana na kundi hilo ambalo mwenyekiti Emanuel Lukumai anasema wameshalitolea taarifa lakini bado hakuna hatua zilizochukuliwa.
ITV imemtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo kwa njia ya simu kuthibitisha tukio hilo ambalo limetolewa taarifa kituo cha polisi Usa River na waliojeruhiwa kupatiwa RB za shambulio la mwili lakini alijibu kwa njia ya ujumbe mfupi kwamba bado hajapokea taarifa na akaahidi kufuatilia kwa ajili ya kulitolea ufafanuzi.
Matukio hayo ya unyanyasaji kwa wanawake yanatokea kipindi hiki ambacho ulimwengu upo kwenye maadhimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia hali inayodhihirisha
No comments:
Post a Comment