Mbali na hili AT amesema kwa sasa yeye yupo likizo katika muziki hivyo hawezi kutoa kazi yoyote mpaka mwakani na kusema yeye na Alikiba ni kati ya wasanii wakali wenye uwezo wa kutunga nyimbo kali na kukaa muda mrefu pasipokuwa na nyimbo na wakafanya poa pindi wanaporudi.
"Bado nipo likizo hadi 2017 kama msanii wako mkali aimbe nyimbo kama 'Nipigie au Makimuga' hadi leo zipo na uhai hadi miaka 50 ijayo. wakati mwingine mashabiki muwe wazima wa akili timamu kufuatafuata mkumbo kwenu siku moja kutawatia kiharusi kuna wasanii hawawezi kukaa hata mwezi kimya ulizeni kwanini? Anaejiamini haogopi wingi wa wasanii anaogopa kufanya kitu chini ya uwezo wake". Aliandika AT
No comments:
Post a Comment