Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo ambazo kila kata imepata pikipiki nane Mrisho amesema kuwa vijana wengi wamekua wakikabiliwa na tatizo la mtaji hivyo pikipiki hizo ni mkombozi katika misha yao ambazo zitawasaidia kukuza mitaji yao na kuongeza kipato chao cha kila siku.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Boda boda jiji la Arusha (UBOJA) ameshukuru Uongozi wa Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Wafadhili waliojitolea kuhakikisha kuwa wanatengeneza fursa za ajira kwa vijana zaidi ya 200 katika jiji la Arusha jambo ambalo litainua vipato vya wananchi wengi.
Dereva wa Bodaboda Dickson Wilbard amesema kuwa mchango huo wa Mkuu wa Mkoa utawasaidia vijana wengi kuacha kukaa vijiweni na kujihusisha na vitendo vya uhalifu na badala yake watakua wachapa kazi.
No comments:
Post a Comment