Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Angellah Kairuki amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (Tasaf), kuwasimamisha kazi maofisa waandamizi watano
wa mfuko.
Maofisa
hao ni wanaosimamia mpango huo pamoja na Meneja wa Uratibu na
Mkurugenzi wa Uratibu kutokana na kushindwa kusimamia mpango wa kunusuru
kaya masikini.
Kairuki
alisema maofisa hao ndio viongozi wasimamizi wakuu wa mpango huo katika
Awamu ya Tatu ya Tasaf na wamesimamishwa kupisha uchunguzi wa jinsi
walivyohusika kuvuruga utekelezaji wa mpango huo hadi kufikia
kuandikisha kaya zisizo na sifa ufanyike.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Kairuki alisema
ameshauriana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi) na tayari ameshaelekeza waratibu wa Tasaf
wa wilaya pia wasimamishwe kazi.
“Nimemwelekeza
Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf awasimamishe kazi mara moja na kuendelea
na hatua nyingine za kinidhamu dhidi ya maofisa washauri 106 walioko
kwenye halmashauri walioshindwa kufuatilia na kusimamia mpango huu mpaka
kusababisha kaya zisizostahili kuingizwa kwenye mpango na kuendelea
kulipwa isivyostahili,” alisema Kairuki.
Aidha
alisema ameagiza ufanyike uchunguzi wa kina kubaini ushiriki wa maofisa
hao na kuchukua hatua stahiki kwa wale watakaothibitika kuhusika.
Aidha
ametaka uchunguzi huo ukamilike ndani ya mwezi. Karuki alisema baada ya
uhakiki kufanyika kaya 55,692 zimeondolewa kwenye mpango kutokana na
sababu mbalimbali ikiwemo vifo, kaya kuhama kijiji, kutojitokeza mara
tatu mfululizo kupokea ruzuku, kuwa wajumbe wa kamati mbalimbali,
wastaafu, viongozi na watumishi wa umma.
Alisema
kuanzia Januari 2014 hadi Septemba 2016, Sh 6,427,110,309 zimeokolewa
kwa kaya 42,035 zilizoondolewa kwa kipindi hicho na kwa kuwa kazi hiyo
ni endelevu kuanzia Oktoba 2016 wakikamilisha kuziondoa kaya
zisizostahili kiasi hicho cha fedha kinaweza kubadilika.
Hata
hivyo amewaagiza Tasaf kuhakikisha wanaendelea kushirikiana na
halmashauri kuongeza udhibiti wa fedha wakati wa malipo na kuhakikisha
fedha zinalipwa kwa kaya zenye sifa peke yake.
Aidha,
amewaagiza Tasaf kuendelea kushirikiana na halmashauri zote kukamilisha
kazi ya uhakiki wa nyumba kwa nyumba katika halmashauri zote nchini
kabla ya malipo yanayofuata ya Januari/ Februari 2017 kufanyika.
No comments:
Post a Comment