Shehe Salum aliyasema hayo juzi Alhamisi (Novemba 1, 2016) alipotembelea Ofisi za Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa Magazeti ya Championi, Uwazi, Ijumaa Wikienda, Ijumaa, Amani na Risasi zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar na kuzungumza na waandishi pamoja na wafanyakazi wa idara nyingine.
Akijibu swali la Mwandishi Aziz Hashim aliyetaka kujua dini inasemaje
kuhusiana na watu kama Diamond kuendelea kuzaa nje ya ndoa, shehe huyo
alisema:
“Niseme tu kwamba hili si kwa Diamond na Zari tu bali kwa wote
wanaofanya zinaa. Dini ya Kiislam inaeleza kuwa, kuzini ni dhambi. Hivyo
kitendo cha Diamond kuendelea kuzaa nje ya ndoa hatakuwa na tofauti na
wanyama wengine ambao nao wanazaliana bila kufunga ndoa.
“Tofauti ya binadamu na wanyama kama mbuzi, ng’ombe au nguruwe ni
kwamba, sisi tunatakiwa kuzaliana baada ya kufunga ndoa, kinyume chake
tutakuwa tunapata dhambi.
“Halafu sasa tukio la kufunga ndoa wala halichukui muda mwingi na halina
gharama kubwa. Ni suala la wahusika kumtafuta tu shehe, anakuja anatia
ubani kisha mnaendelea na maisha yenu. Kama ni kutumia pesa itakuwa ni
elfu hamsini tu au laki moja.
“Labda niseme tu kwamba, hata mimi kama kweli wamedhamiria kufunga ndoa,
niko tayari kuwaozesha bure kabisa, nitaweka gari yangu mafuta
kuwafuata popote, wao wajipange tu wakiwa tayari wanitafute.”
Shehe huyo aliongeza kuwa, anaona litakuwa jambo jema kwa wawili hao
kuoana kwani kuendelea kuzaa nje ya ndoa ni kuwakosesha haki watoto wao
hasa ile ya kurithi mali.
No comments:
Post a Comment