SLIDE MANENO
Sunday, January 22, 2017
POLISI DAR KAZI WANAYO
Mashabiki wa simba watunisha vifua na kudai kuwa timu ya polisi Dar es salaam leo kazi wanayo.
VINARA wa Ligi Kuu Soka Tanzania bara Simba leo wana kibarua kizito cha kusaka ushindi katika mchezo wa raundi ya tano wa Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya timu ya Ligi Daraja la Kwanza Polisi Dar es Salaam.
Mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa Uhuru, huku pia Ruvu Shooting ikiwakaribisha timu ya daraja la kwanza Kiluvya United kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi katika mechi ya michuano hiyo.
Aidha, Toto Africans itacheza dhidi ya Mwadui kwenye uwanja wa CCM Kirumba na timu ya Daraja la pili Mbeya Warriors ikicheza dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Simba inachukulia mchezo huo kwa umuhimu kwao kufanya vizuri ili kuingia katika hatua nyingine na hasa ikizingatiwa bingwa wa michuano hiyo anapata nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.
Kocha Msaidizi wa wekundu hao wa Msimbazi Jackson Mayanja alisema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi.
"Katika mchezo wowote hatuamini kama kuna timu ndogo, tunauchukulia kwetu ni muhimu tutapambana kushinda,"alisema.
Meneja wa Simba Mussa Mgosi alisema wanakabiliwa na majeruhi Mohamed Ibrahim hivyo, uwepo wake itategemea na maendeleo yake kiafya.
Katika msimu uliopita Simba iliishia hatua ya robo fainali baada ya kufungwa na Coastal Union.
Kocha Mkuu wa Polisi Dar es Salaam Ngero Nyanjabha alisema Simba ni timu kubwa na wanaiheshimu, na kwamba huenda mchezo ukawa mgumu, ni lazima wapambane kupata matokeo mazuri.
Alisema kikosi chake kiko vizuri kwasababu kilikuwa kwenye ligi na wanaamini wanaweza kupata matokeo mazuri.
Kwa upande wa Ruvu Shooting, Msemaji wake Masau Bwire alisema kikosi hicho kilikuwa kwenye mazoezi ya muda mrefu kinaamini kitapata ushindi dhidi ya Kiluvya United
Labels:
BURUDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment