Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kupata pigo
baada ya wanachama 200, wakiwamo viongozi wa Kitongoji cha
Kwemghogho Mahezangulu kujitoa na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi
(CCM) .
Akizungumza
baaada ya kupokea wanachama hao, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba
(CCM), alisema wananchama hao wameamua kurudi wenyewe nyumbani
kutokana na kuona ahadi nyingi za maendeleo zimetekelezwa kwa
kiasi kikubwa.
Alisema chama chake kimefanya mambo mengi hivyo haoni ajabu ya kupokea wanachama kutoka vyama vingine vya upinzani.
January,
ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia
Muungano na Mazingira, alisema hivi sasa kuna kazi kubwa ya kuendelea
kuleta maendeleo ambayo yanahitaji umoja na mshikamano.
Alisema
migogoro, majungu na fitina inatokana na kambi zilizokuwapo huku
akiwasisitiza wana CCM watambue ni hema kubwa na linavumilia tofauti za
watu.
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chadema Kitongoji cha Kwemghogho, Shabani Kahema,
aliwataka vijana na wanachama wengine kubadilika kwa kuwa CCM
ndiyo chama chenye ilani inayotekelezeka.
No comments:
Post a Comment