Naibu
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo ndugu Msafiri A Mtemelwa ametoa taarifa
kuwa kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Mh Zitto Kabwe hajakamatwa na
polisi na kusema yupo salama hapa hapa nchini.
Akitumia
mtandao wa twitter wa Chama cha ACT Wazalendo Msafiri Mtemelwa anadai
kuwa kiongozi huyo wa chama yupo salama lakini dereva wake ndg Patrick
Muhidin pamoja na katibu wa Chama wa jimbo la Kahama ndg. Vincent
Ikerenge ndio walikamatwa na walipelekwa kituo cha polisi Kahama na
kuandikishwa maelezo.
"Tunawajulisha
kuwa kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo ndg. Zitto Kabwe, Mb
hajakamatwa na polisi na yupo salama hapa hapa nchini. Tarehe
21/1/2017 Polisi wilayani Kahama wakiwa na magari 7 kati yao manne ya
FFU walivamia mkutano wa Kampeni wa Chama katika kata ya Isagehe,
Halmashauri ya Mji wa Kahama. Kiongozi wa Chama alikuwa jukwaani wakati
polisi wanafika na aliendelea na hotuba yake mpaka mwisho na kumnadi
Mgombea ndg Ibrahim Masele. Baada ya kushuka jukwaani, Kama kawaida yake
alipeana mikono na wananchi na baadaye alipotea katika eneo Hilo" alisema Msafiri Mtemelwa
Kwa
mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo ndugu Msafiri Mtemelwa
anadai wamefuatilia polisi kutaka kujua kwanini kiongozi wa Chama chao
anatafutwa na polisi na kusema wamejulishwa kuwa ana mashatka ya kutoa
lugha ya uchochezi katika hotuba zake za kampeni.
"Tumejulishwa
na polisi kwamba Kiongozi wa Chama ana mashtaka ya kutoa lugha ya
uchochezi katika hotuba zake za kampeni katika kata ya Isagehe Jimbo la
Kahama Mjini. Polisi wanasema Zitto Kabwe amemchonganisha Rais na
wananchi kwa kusema kuwa Rais anakula bure na kulala bure ndio maana
hajali hali ngumu ya maisha ya wananchi wakati huu wa balaa la njaa" ameandika Mtemelwa
Hata
hivyo mbunge huyo wa Kigoma mjini na kiongozi wa Chama cha ACT
Wazalendo kupitia viongozi wa chama cha ACT Wazalendo amesema polisi
wataweza kumkamata iwapo yeye atataka kukamatwa na siyo kwa kuvamiwa
bali kwa kuitwa rasmi na polisi na kuelezwa makosa yake.
"Chama
kinalitaka jeshi la polisi kufuata taratibu za kukamata raia kwa mujibu
wa sheria na pia protokali za kuwaita polisi viongozi wa Kitaifa Kama
ilivyo kwa ndg Zitto. Chama kinajiandaa na wanasheria wake ili kwenda na
KC kituo chochote cha polisi nchini Mara watakapopata wito wa kwenda
polisi.". Amesema Msafiri Mtemelwa
No comments:
Post a Comment