(picha na Nickson Sawe)
Body ya michezo imejibu maswali mbalimbali ya wadau wa michezo mbalimbali katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha A.J.T.C
(picha na Nickson Sawe)
Naibu waziri wa michezo wa serikali ya wanafunzi katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha amejibu maswali ya wanafunzi wa chuo hicho yaliyohusu majukumu ya Mr na Mrs A.J.T.C ambapo ameeleza majukuma ya watu hao ikiwa ni pamoja na kukitangaza chuo katika maeneo mbalimbali kupitia mitandao yao ya kijamii na pia kuwa mfano wa kuigwa kupitia tabia na ubunifu wao katika mambo mbali mbali ikiwemo Mitindo.
(picha na Emanuel Njiro)
Mr A.J.T.C anayekaribia kumaliza muda wake Bw Barack Lang akijibu swali la mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho Bw Yusuph Benjamin ameeleza mambo mengi aliyoyafanya katika kipindi chote ikiwa ni pamoja na kutangaza chuo na pia bado yupo katika mikakati ya kukiunganisha chuo hicho na wanamitindo maarufu.
(picha na Emanuel Njiro)
Bw Kaleb Rafael ambae pia ni mwanafunzi chuoni hapo alihoji kuhusu michezo ya kutoka nje ya chuo hicho kwaajili ya kujenga mahusiano mazuri na watu na bodi hiyo ilimjibu kuwa kusema imeanza kufanya jitihada za kuboresha suala hilo. Bw Rafael pia amewahi kuwa kocha wa kikosi cha certificate na kutikisa kikosi cha diploma hata kutwaa taji la kreti za soda zilizogonganisha timu hizo.
(Picha na Nickson Sawe)
(picha na Nickson Sawe)
Chuo hicho kinapatikana mkoani arusha Kina historia ya kushinda Vikombe mbalimbali licha ya hali ya kimichezo kuonekana kuzorota kwa sasa chuoni hapo, na pia ni chuo namba moja kwa ubora kati ya vyuo vyote vya kati vya uandishi wa habari na utangazaji Tanzania.MPANGO MZIMA WA BURUDANI.
Wasanii mbalimbali na Dj Mafekeche pia walidondosha bonge la show katika ishu hiyo nzima ya kiburudani
kiujumla kuona video nzima bofya link hapa
https://www.facebook.com/nickson.sawe.37/videos/1884454045176143/
HABARI NA
NICKSON SAWE
No comments:
Post a Comment