Ndani ya siku hizi mbili kumekuwa na habari mbali mbali kuihusu Manchester United.Moja ya habari kubwa ni kufungiwa kwa mshambuliaji wa timu hiyo Zlatan Ibrahimovich.Zlatan ameadhibiwa na FA kutocheza michezo mitatu inayohusisha chama hicho cha soka nchini Uingereza.Michezo hiyo inahusiana na chama cha FA tu na haihusiani na Europa.
Adhabu ya Zlatan inakuja baada ya kufanya vitendo visivyo vya kiungwana wakati wa mchezo kati ya Manchester United dhidi ya Fc Bournamouth.Katika mchezo huo Zlatan alionekana akimpiga kiwiko Tyrone Mings wa Bournamouth tukio ambalo muamuzi hakuliona lakini FA kupitia picha za video wameamua kumuadhibu Zlatan na sasa atakosa mchezo wao mgumu wa robo fainali ya FA dhidi ya Chelsea.Lakini pia Zlatan atakosa mechi ya United dhidi ya Midllesbrough na ile dhidj ya West Bromich Albion.
Hapo hapo United,kikosi chao kimesafiri kwenda nchini Urusi kukabiliana na Fc Rostov ya nchini humo.Katika msafara huo United wamemuacha Wayne Rooney na Luke Shaw nchini Uingereza.Lakini wakati Shaw na Rooney wakiachwa Uingereza Henrikh Mkhitaryan amerejea kwenye timu baada ya majeruhi na ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri kwenda Urusi.United tayari wameanza kuonywa kuhusu usalama nchini Urusi,ambapo mashabiki wameshauriwa kuepuka kavaa jezi za timu yao wakiwa peke yao matembezini nchini humo.Fc Rostov ni kati ya timu zenye mashabiki wakorofi sana nchini Urusi.
Marcos Rojo yupo kwenye kikosi kilichoenda Urusi pamoja na kufiwa na binamu yake siku ya Jumatatu nchini kwao Argentina.Marcos alionekana akitokwa na machozi alipokuwa uwanja wa ndege na inasemekana wakati anajiandaa na safari ndipo aliposikia habari za kumhusu binamu yake huyo.Haijawekwa wazi kama Rojo atakuwa tayari kucheza dhidi ya Rostov au anaweza kupumzishwa.
No comments:
Post a Comment