Leo Ikulu jijini Rais Magufuli alimuaga gavana anayemaliza madaraka yake, Beno Ndulu na kumkaribisha Luoga. Baada ya maagano amesema amepanga kuanzia mwezi ujao kulipa madeni ya ndani ikiwemo ma-suppliers wa chakula kwenye shule na vyuo pia contractors kwani kwa sasa uchumi unaenda vizuri sana na kuna pesa nyingi.
Rais Magufuli pia amesema yapo madeni ya wafanyakazi kama walimu na kutaka madeni yote ya wananchi yalipwe na atatoa bilioni 200 zikalipe. Amedai angeweza kutoa hata kesho lakini uhakiki upite kwanza na wakimaliza mapema amemruhusu gavana azitoe.
Amesema anaamini zitawasaidia wananchi kwa sababu bilioni 200 sio kitu kidogo kuzitoa kwa pamoja na wadeni wote wa ndani wanaoidai serikali walipwe.
Magufuli amesema anaamini magavana watakubaliana nae hio ni njia mojawapo ya kuboost(Kuhuisha) uchumi kwani bilioni 200 zinazotolewa zitasambaa kwa wananchi na gavana anaechukua madaraka alisimamie vizuri.
No comments:
Post a Comment