SLIDE MANENO
Friday, March 31, 2017
Hatari!!! Kutembea mwisho saa 3 usiku
mkoa wa Pwani hali ni tete baada ya viongozi wa serikali za vijiji kuuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana ambao mpaka ninapo andika taarifa hakuna aliyekamatwa.
Kuna viongozi takribani watatu serikali za vijiji wamepoteza maisha yao na wahusika hawajakamatwa bado, hali hiyo imepelekea watu wa Ikwiriri, Kibiti, Njopeka kutembea mwisho saa 3 usiku
Nadhani huu ni muendelezo wa majambazi ambayo yalikamatwa vikindu na moja lilitoroka baada ya kumuua kiongozi wa msafara katika shambulio hilo.
Kwa mjibu wa baadhi ya jamaa waliotembea maeneo hayo wanadai kuwa askari wamemwaga sana katika eneo hilo lakini ajabu ni kwamba bado mauaji yanaendelea.
Inasemekana usiku wa kuamkia juzi majambazi hayo yalipanga magogo katika kona ya kuelekea Hospital ya Songa na kupora wasafiri vitu mbalimbali ikiwa pamoja na fedha wakitumia mapanga na kuwajeruhi wasafiri takribani 8 ambao wamelazwa Hospital ya Songa.
USHAURI KWA SERIKALI.
Tanzania imekuwa ni nchi ambayo ulinzi wa mipakani ni dhaifu sana kiasi ambacho wageni wanaweza kuingia na kutoka kadri wanavyoweza bila ya shida yeyote hivyo nashauri serikali iimarishe ulinzi wa mipakani.
USHUHUDA.
Nimewahi kisafiri kutoka Nairobi kupitia Namanga na kutoka Mombasa kupitia Holili unapokuwa Kenya au Uganda wenzetu wako makini basi linaposamishwa basi katika vizuizi wanakagua kila mtu kitambulisho lakini ukiingia huku kwetu wanakagua kwa kutazama sura.
SIYO INCHI YA AMANI TENA.
Tanzania siyo ichi ya amani tena kama majambazi yaliweza kuvamia vitu vya polisi Ikwiriri Kimanzichana na baadaye Sitaki shari katikati ya jiji bila kukamatwa tunatarajia nini ni kweli tuko salama hapana.
Serikali imechukua hatua gani kukabiliana na uhalifu huu jibu ni kwamba hakuna bado tumebweteka tuu Tanzania sasa hivi unaweza kuizunguka yote kwa kutumia gari dogo kutoka na miundombinu ilivyoboreshwa.
WAKIMBIZI.
Nchi hii sasa hivi imejaa wakimbizi kila kona lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na wakimbizi hawa wanatoka katika nchi ambazo haziko salama kabisa asilimia kubwa ya wanaofanya biashara ya matunda ni wakimbizi kutoka Burundi na Rwanda na hata wale ambao wanauza kahawa pia asilimia kubwa ni wakimbizi.
Magereji ya magari hasa ya watanzania wenye asili ya kisomali yanahifadhi wakimbizi wa kisomali magodown yote yamejaa wahindi maafisa uhamiaji wakienda kazi yao kubwa ni kuchukua rushwa na kurudi.
Tumeshuhudia juzi hapa watanzania waliokuwa wakiishi nchini msumbiji bila ya utaratibu wakirejeshwa sisi tunangoja nini ujambazi utaishaje?
Viongozi pangeni mkakati wakuifanya Tanzania endelee kuwa na amani hali iliyopo sasa inatisha kuna kipindi ujambazi ulikuwa unatisha lakini IGP Mwema alifanya kazi kubwa kuutokomeza IGP Mangu kaza buti vinginevyo kazi inakushinda.
Labels:
HABARI KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment