Maelfu ya maduka yatasitisha uuzaji wa vinywaji vya Coca-Cola na Pepsi kuanzia Jumatano hii ni katika jimbo la Tamid Nadu nchini India
Mashirika mawili ya biashara yametoa wito kwa washirika wake kususia kuuza vinywaji vya kigeni na badala yake kukuza bidhaa zinazotengezwa nchini humo.
Wameshutumu kampuni za vinywaji hivyo kwa kutumia vibaya maji nchini humo wakati ambapo wakulima wanakabiliwa na hali ngumu ya ukame.
Hatua hiyo pia inaangazia ushawishi wowote wa kigeni nchini humo.
Shirika moja linaloshirikisha kampuni za Coke na Pepsi, na shirika la vinywaji nchini humo zimedai kusikitishwa sana na hatua hiyo
No comments:
Post a Comment