asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Thursday, December 22, 2016

Godbless Lema augua ghafla gerezani......ashindwa kufanya haya


Kesi iliyokuwa isikilizwe 21 Disemba 2016 inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema pamoja na mkewe, Neema Lema wakituhumiwa kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo imeahirishwa kutokana na hali ya Godbless Lema kuwa mbaya gerezani.

Taarifa za Godbless Lema kushindwa kufika mahakamani zimetolewa na wakili wa serikali Elizabeth Swai kwa Hakimu Mfawidhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Augustino Rwezile ambapo alisema kuwa alipata taarifa kutoka kwa Afisa Magereza zikieleza kuwa mbunge huyo anaumwa na amepewa mapumziko hivyo asingeweza kufika mahakamani.

Aidha, taarifa kutoka kwa kiongozi huyo wa magereza hazikueleza wazi kuwa mbunge huyo anaugua ugonjwa gani.

Kuhusu kesi hiyo inayowakabili wanandoa hao wawili jana  walikuwa wasomewe hoja za awali ambapo pia shahidi wa kwanza kutoka upande wa Jamhuri, George Katabazi alikuwa atoe ushahidi.

Godbless Lema na Neema Lema wanakabiliwa na kesi ya kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha kitendo wananchodaiwa kuwa walikitenda kupitia ujumbe mfupi wa simu mara baada ya Rais Magufuli kumteua Mrisho Gambo kuuongoza mkoa huo.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt