asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Tuesday, July 11, 2017

BUNDI ANGURUMA TENA JANGWANI.,..!! LWANDAMILA, AJIBU NA NINJA WAZUA KITENDAWILI KIPYA YANGA, TAZAMA HAPA ILIVYOKUWA



Yanga itaanza mazoezi kujinoa chini ya Kocha Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina, kesho badala ya leo kama ilivyotarajiwa.

Hii ni baada ya kusogeza ratiba kwa siku moja baada ya wachezaji wake kadhaa akiwemo Ibrahim Ajibu, Abdallah Shaibu 'Ninja' na Pius Buswita kutofika katika upimani huo wa afya ambao wanafanyiwa wachezaji wote.

Ajibu amejiunga na Yanga hivi karibuni akisaini mkataba wa miaka miwili akitokea Simba baada ya mkataba wake na Mnyama kumalizika mapema mwezi huu.

Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema timu hiyo ilitarajiwa kuanza mazoezi ya kujiandaa na Ngao ya Jamii na Ligi Kuu Bara leo Jumatatu lakini kutokana na baadhi ya wachezaji kutojitokeza kwenye zoezi la upimaji wa afya zao, kocha ameona asogeze mbele.

Saleh alisema, timu hiyo itaanza mazoezi yake ya pamoja kesho Jumanne asubuhi kwenye uwanja watakaoutangaza mara baada ya kuupata.

Aliongeza kuwa, sababu nyingine ya mazoezi hayo kusogezwa mbele ni kutokana na baadhi ya wachezaji kuchelewa kurejea jijini Dar es Salaam baada ya kwenda likizo.

"Mazoezi rasmi ya pamoja kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mechi ya Ngao ya Jamii na msimu mpya wa ligi kuu hayatafanyika tena kesho (leo Jumatatu) kama tulivyopanga awali.


“Kocha alitoa maelekezo kwa uongozi kuwa anataka kuona wachezaji wote wanapima afya zao kabla ya kuanza mazoezi na tayari baadhi ya wachezaji wameshapima," alisema Saleh.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt