asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Wednesday, December 7, 2016

TETEMEKO LAUA WATU NA KUSABABISHA UHARIBIFU INDONESIA TAZAMA HAPA

 Majumba kadha, ikiwemo misikiti, yameporomoka

Tetemeko kubwa la ardhi limeua watu zaidi ya 24 na kusababisha uharibifu mkubwa katika mkoa wa Aceh nchini Indonesia.

Maafisa wanasema watu wengi wamefukiwa kwenye vifusi vya majumba yaliyoporomoka.

Tetemeko hilo la nguvu ya 6.4 kwenye vipimo vya Richter lilitokea karibu na mji wa Sigli katika kisiwa cha Sumatra ambapo majumba mengi yameporomoka.

Shirika la utabiri wa hali ya hewa la Indonesia limesema hakuna hatari ya kutokea kwa kimbunga.
Mwaka 2004, mkoa wa Aceh uliathiriwa sana na kimbunga kilichosababishwa na tetemeko kubwa baharini. Watu 120,000 waliuawa mkoani humo.

Vimbunga vinavyopewa majina duniani
Taasisi ya Jiolojia ya Marekani imesema tetemeko hilo lilitokea karibu na pwani mwendo wa saa 11:03 asubuhi saa za huko (22:03 GMT Jumanne) katika kina cha 17.2km (maili 11) chini ya ardhi.

Said Mulyadi, naibu mkuu wa wilaya ya Pidie Jaya, eneo lililoathiriwa pakubwa na tetemeko hilo, ameambia idhaa ya BBC ya Indonesia kwamba huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.
 Maafisa wanahofia huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka kwani watu wengi wamefukiwa kwenye vifusi vya majumba yaliyobomoka
 Maafisa wa uokoaji wanawatafuta manusura

Maafisa wamesema huenda kusitokee kimbunga


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt