asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Wednesday, December 7, 2016

TFF YAPIGA MARUFUKU WAAMUZI WA NJE

OFISA HABARI WA SHIRIKISHO HILO, ALFRED LUCAS.

SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), limesema haliwezi kuruhusu klabu kuleta mwamuzi kutoka nje ya nchi kuja kuchezesha mchezo wowote kwa kuwa katiba na taratibu haziruhusu.
Ofisa habari wa shirikisho hilo, Alfred Lucas, alisema maombi ya klabu ya Simba hayawezekani kwa kuwa Katiba ya TFF hairuhusu.

"Suala hilo haliwezekani kwa sababu kwanza kama tunataka kufanya hivyo ni lazima hata kanuni zetu za ligi zibadilike kwanza, kwa sababu kanuni zinawatambua waamuzi wa ndani," alisema Lucas.

Kauli hiyo ya TFF imekuja siku chache baada ya Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kusema klabu haitakuwa tayari kuingiza timu uwanjani kwenye mchezo wowote dhidi ya Yanga kama haitachezeshwa na waamuzi kutoka nje.

Manara, alisema klabu hiyo ipo tayari kuingia gharama za kuleta mwamuzi wa nje ya nchi kwa ajili ya mechi zote dhidi ya watani wao hao.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt