asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Thursday, February 9, 2017

HARUSI YA DIAMOND NA ZARI YAPANGWA KUWA HIVI

Zari The Bosslady amedai kuwa anataka harusi yake na Diamond Platnumz iwe kubwa na yenye gharama kuwahi kufanyika Afrika Mashariki.

Hata hivyo, itafanyika baada ya kuwa wamefanya mambo ya muhimu zaidi ikiwemo kujijenga zaidi walivyo sasa. Akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Alhamis hii, Zari amedai kuwa suala la kufunga ndoa sio kitu kinachowapa pressure.
Amedai kuwa hawajawahi kukaa chini na kuwa na majadiliano ya kina kuhusu ndoa, licha ya hadi sasa kuwa na watoto wawili, Tiffah na Nillan. Staa huyo wa Uganda amedai kuwa moja ya mambo ambayo wanataka kufanya ni kuhakikisha kwanza wanawajengea watoto wao apartments zao zitakazowasaidia katika maisha yao hata kama wazazi wao wasipokuwepo.
Hata hivyo Zari amedai kuwa mwezi March mwaka huu Diamond ataenda rasmi kujitambulisha kwa baba yake na kuhalalisha uhusiano wao pamoja na kuomba mkono wa ndoa.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt