
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ametaja kasoro kadhaa katika
zoezi la vita ya dawa za kulevya lililoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam Paul Makonda.
Amesema, Kwanza,
Mkuu wa Mkoa hana mamlaka yoyote ya kuelekeza watu kwenda kuripoti
polisi. Hii ni licha ya mamlaka yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Mkoa na mamlaka yake ya kipolisi yapo chini ya Sheria ya
Tawala za Mikoa.
Pili, kwa mujibu
wa Sheria ya Mwenendo wa Jinai, kila mtu ana wajibu wa kutoa taarifa ya
kosa la jinai analoona limetendeka kwa polisi. Hii ni ile inayoitwa
kufungua RB. Mkuu wa Mkoa Makonda alitakiwa afungue RB kwa wote
anaowatuhumu kufanya biashara ya madawa. Hajafanya hivyo na ni kosa la
jinai kutokufanya hivyo.
Tatu, kwa
kutumia mamlaka yake ya kipolisi, Mkuu wa Mkoa Makonda alikuwa na uwezo
wa kuamuru wale wote anaowatuhumu kufanya biashara ya madawa kukamatwa
na kuwekwa kizuizini kwa masaa 48 na baadae kufikishwa mahakamani.
Badala ya kuamuru 'wahalifu' hawa wakamatwe, Mkuu wa Mkoa Makonda
aliwaelekeza wajipeleke polisi kwa mahojiano.
Nne, kwa
kuzingatia hatari kubwa ya madawa ya kulevya kwa jamii yetu, sheria
husika za nchi zimeweka adhabu ya chini kabisa ya kifungo cha miaka 20
kwa wanaothibitika na mahakama kuhusika na biashara hiyo. Aidha, makosa
ya madawa ya kulevya hayana dhamana kisheria. Iweje wale wote
waliotuhumiwa na Mkuu wa Mkoa Makonda wamepelekwa mahakamani lakini wote
wamepewa onyo tu au wamepewa dhamana Mahakamani.
Kati ya mapolisi 11 waliotuhumiwa, hakuna hata mmoja aliyepelekwa
mahakamani na kushtakiwa kwa tuhuma hizi. Badala yake, tunaambiwa
wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa polisi dhidi yao. Kwa mujibu wa
Sheria zetu za ajira, mtumishi anayesimamishwa kazi analipwa mshahara
kamili kwa muda aliosimamishwa
Usikose pia habari hzi...bofya hapa chini
MAKONDA ATUPILIA MBALI WITO WA BUNGE, AAMUA HAYA...soma hapa..}}}}}}}
VIDEO: ZARI AONYESHA UWEZO WAKE WA KUKATA MAUNO KATIKA 40 YA MTOTO WAKE NA DIAMOND...itazame hapa.. }}}}}
VIDEO: ZARI AONYESHA UWEZO WAKE WA KUKATA MAUNO KATIKA 40 YA MTOTO WAKE NA DIAMOND...itazame hapa.. }}}}}
No comments:
Post a Comment