
Rais wa Jamhuri ta
Tanzinia Dkt John Magufuli, ameviagiza vyombo vyote vya ulinzi na
usalama kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa
kuhakikisha vinasimamia sheria ipasavyo ili kukabiliana na tatizo hilo
nchini humo.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo hii leo katika Ikulu
ya mjini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuwaapisha Kamishna mkuu wa
mamlaka ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya Bwana Rogers Siyanga,
Kamishna Jenerali wa uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala, Balozi wa
Tanzania nchini Ubelgiji Mheshimiwa Joseph Sokoine, Balozi wa Tanzania
nchini Algeria Mheshimiwa Omar Yusuf Mzee na Balozi wa Tanznia nchini
Uganda Mheshimiwa Grace Aaron Mgovano#Dkt Magufuli amewataka viongozi wote wa serikali kuungana na vyombo vya dola katika mapambano dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya, na ametaka mapambano hayo yasifanywe kwa mzaha wala kwa kuangalia majina ya watu, vyeo vyao na taasisi wanazoongoza.
Mheshimiwa Magufuli amrwapongeza viongozi wote wa mikoa walioanza kukamata watu wanaojihusisha na biashara za dawa za kulevya, na amewaomba Watanzania wote waunge mkono juhudu za kukabiliana na wanaofanya biashara na kutumia dawa za kulevya, ambazo zinazidi kuangamiza nguvu kazi ya taifa.
usikose pia habari hii.......
LISSU AMPINGA MAKONDA KWA HOJA NZITO TANO(5): SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA {{{{{bofya hapa}}}}}
No comments:
Post a Comment