Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameonekana
kwenye ukurasa wake mtandao wa instagram akiwa na msanii Khalid Mohamed
‘TID’ ambaye siku chache zilizopita alimtaja katika orodha ya watuhumiwa
wa kujihusisha na dawa za kulevya.
Baada ya kutajwa, TID akiwa na wasanii kadhaa waliotajwa na mkuu huyo wa
mkoa walifika Kituo Kikuu cha Polisi jijini humo na kuhojiwa kisha
kuachiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu lakini ikiwa ni baada ya
kuwekwa chini ya uangalizi wa mwaka mmoja.
Kuonekana kwa Makonda akiwa na TID kumeibua mijadala kuwa huenda ameanza
kukutana na watu aliowataja kutumia dawa za kulevya ili kutatua tatizo
hilo.
Kupitia ukurasa wake wa instagram, Makonda ameweka picha inayomuonyesha akiwa na msanii huyo.
Pamoja na picha hiyo, Makonda ameandika “Mungu wetu hajalala na siku zote anampenda amtafutae, karibu tena nyumbani TID”.
Picha hiyo pia inaonekana kwenye ukurasa wa instagram wa TID ikiwa na
maneno “muziki bila dawa za kulevya inawezekana....This is the turning
point kwangu mimi na kizazi cha muziki huu wa kizazi kipya, nikiwa na
Mh. Makonda leo tukijadili jinsi ya kuokoa vipaji na sanaa kwa ujumla,
Mungu ibariki Bongo fleva, Mungu ibariki Tanzania”.
SLIDE MANENO
Sunday, February 12, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment