asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Friday, February 24, 2017

RIHANA NAYE AGUSA ALIPOGUSA MICHAEL JACKSON

Rihanna
Haki miliki ya pichaMAGES

Rihanna amegusa alipogusa msanii nguli Michael Jackson hii ni baada ya hit maker huyo wa wimbo wa love on the brain kutoka huko nchini marekani kumfikia Michael Jackson kwa kuwa na nyimbo katika chati ya nyimbo kumi bora nchini Marekani.
Hii ni baada ya wimbo wake mpya wa Love on the Brain kuingia kwenye orodha hiyo.
Wimbo huo ni wake wa 30 kuwa kwenye chati hiyo, na sasa ameachwa nyuma na The Beatles na Madonna pekee.
Madonna ana nyimbo 38 zilizowahi kuwa kwenye chati hiyo. The Beatles wana nyimbo 34.
Jackson, aliyefariki Juni 2009, alikuwa na nyimbo 29 katika chati hiyo ya nyimbo kumi bora.
Mwaka 2005, wimbo wa Rihanna wa Pon De Replay ulikuwa namba mbili katika chati za muziki Marekani na Uingereza.
Imemchukua miaka 10, miezi saba na wiki mbili kuwa na nyimbo 30 kwenye chati ya nyimbo bora Marekani.
Nyimbo zilizovuma za Madonna alizichomoa katika kipindi cha miaka 13.



MadonnaHaki miliki ya picha
Image captionRihanna alimfikia Madonna orodha ya waimbaji wa kike wenye nyimbo nyingi zaidi chati ya 100 bora Marekani Julai 2016

The Beatles walifika hapo kwa kutumia miaka mitano, miezi tisa na wiki mbili pekee.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt