asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Friday, February 24, 2017

WEMA SEPETU AFUNGUKA WAZI WAZI KUHUSU FEDHA ZA KAMPENI ANAZODAI CCM

Malkia wa filamu nchini Wema sepetu amethibitisha kuwa japo amekihama Chama cha Mapinduzi lakini bado alikuwa anadai madeni yake yaliyotokana na kampeni za uchaguzi mkuu alizofanya mwaka 2015 akiwa na wasanii wengine.
Image result for wema sepetu chadema
Akiongea mbele ya waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wanachama wa Chadema leo hii, Wema amesema walikuwa wanakidai chama hicho yeye na wasanii wenzake wengine lakini wamekuwa wakiambia madeni hayo wakamdai Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.
“Kuna madeni kweli ambayo wasanii wenzangu wanadai nikiwemo mimi lakini cham kama chama kinajua chenyewe, nikianza kuongelea madeni nitakuwa kama nakumbuka shuka asubuhi,” amesema Wema.
“Madeni yapo kama hilo ndio swali na wasanii wenzangu wengi wanakidai Chama cha Mapinduzi lakini sasa tumekuwa tunaambiwa tumfuate tumfuate JK. Tumfuate JK tukamdai na maneno mengine mengi ambazo ni fununu tumekuwa tunasikia,” ameongeza.
Kwa sasa Wema na mama yake ni wanachama wa Chadema
USIKOSE PIA HABARI HIZI........








No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt