asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Friday, February 24, 2017

MZEE WA UPAKO AMCHANA LIVE NEY WA MITEGO "SIO UTATEMBELEA NDALA UTATEMBELEA KUCHA"


Baada ya hivi karibuni msanii wa hip hop, Nay wa Mitego kutangaza kuwa atafungua kanisa lake ambalo litakuwa si la biashara bali ni la kumuabudu Mungu aliye hai, Mchungaji maarufu nchini, , Lusekelo Anthony aka Mzee wa Upako amemuonya kutomchezea Mungu.

Mzee wa upako ameyasema hayo alipotafutwa na E-News ya EATV baada ya kuulizwa maswali juu ya kauli hiyo.

“Kama unakuja kanisani kwa maana kuna biashara, nakupa miaka hii mitatu sio utatembelea ndala utatembelea kucha, ni mtoto mdogo sana hana akili. Mungu hataniwi, anafanya kufuru, kama ana mama yake amemzaa amuonye. Mimi biblia nimesoma na hizo lugha zake nyepesi zitamtokea puani, asithubutu kufanya kanisa kama biashara. Baada ya miaka hii mitatu atajua kwamba kuongoza watu sio kama kuongoza ngo’mbe hakuna jambo gumu kama kuongoza watu wenye akili kama wewe wenye ufahamu kama wewe, wapo watu wengi walianzisha makanisa kwanini walifunga, ujinga hujui ni ujinga ni utoto,” Alisema Mzee wa Upako.



No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt