asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Friday, February 24, 2017

AUDIO: MAZUNGUMZO YA SIMU YA MAGUFULI NA MWANAMKE ALIYEMWAGIWA UJI WA MOTO NA MUMEWE YAWATOA WATU MACHOZI

Rais Dkt John Pombe Magufuli, amempigia simu mwanamke aliyemwagiwa uji wa moto na mume wake huko Mara. Mazungumzo hayo yamewatoa watu machozi kwani yanatia huruma.

Neema Mwita Wambura akizungunza Rais Magufuli na kumshukuru kwa msaada aliompatia wa kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Neema Mwita Wambura (32) alimwagiwa uji wa moto ukiwa unachemka jikoni na mume wake katika kijiji cha Kyagata,Tarime mkoani Mara baada ya mume huyo kukasirika kwasababu Neema alichuma mahindi mabichi na kuyapika bila kibali cha mumewe.
Baada ya hapo majeraha yamekuwa yakimsumbua mno katika mwili wake.
Rais Dkt John Magufuli aliingiwa na huruma baada ya kumuona Neema, na alimpigia simu pamoja na kuwaagiza watu kumpatia fedha za matibabu pamoja na kumjulia hali yake.
Rais Magufuli ameahidi kumpatia hifadhi mama huyo pamoja na watoto wake watatu ambao kwa sasa wapo Bunda mkoani Mara. Pia alimpatia msaada wa shilingi laki tano.
USIKOSE PIA HABARI HIZI.........






No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt