asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Wednesday, March 15, 2017

Baada ya kukaa kimya tangu sakata la madawa ya kulevya lianze, Diamond Aamua Kumchana Makonda Ukweli wa Moyo Wake..!!!


MSANII  wa muziki wa Bongo Fleva,  Nasib Abdul ‘Daimond Platnumz’, ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa "mary you" aliomshirikisha Neyo, amekaa kimya toka sakata la unga lianze ila sasa amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda kwa jitihada zake kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa salama.

“Kwanza kabisa Nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda kwa jitihada zake. Ukizingatia ni mwaka mmoja tu tokea awe mkuu wa mkoa lakini utendaji wake umezaa matunda mengi na changamoto ni nyingi zinazo mkabili lakini bado amekuwa imara.”, alisema Diamond.

Diamond ameyasema hayo leo katika mkutano  kuhusu vita dhidi ya madawa ya kulevya uliofanyika katika Bwalo la Polisi Oster Bay jijini Dar es Salaam ambako Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na viongozi wengine wa serikali na taasisi mbalimbali walihudhuria.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt