asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Thursday, March 16, 2017

FA waishtaki Manchester United

Klabu ya Manchester United imeshtakiwa na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kosa la kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake wakati wa mechi ya robo fainali ya kombe la FA siku ya Jumamosi dhidi ya Chelsea.
Mwamuzi Michael Oliver alizungukwa na wachezaji wa United baada ya kumpa kadi nyekundu Ander Herrera dakika 10 kabla ya muda wa mapumziko.
United walifungwa mechi hiyo 1-0.
Taarifa ya FA ilisema kuwa imewapa United hadi saa kumi na mbili jioni saa za Uingereza kuwa wameshajibu.
Herrera ambaye ni kiungo wa kati ambaye ni raia wa Hispania alitolewa nje baada ya kumchezea visivyo kwa mara ya pili mshambuliaji Eden Hazard.
Hakuna hatua zaidi itakayochukuliwa dhidi ya Marcos Rojo kwa kisa alichofanya katika dakika za mwisho za mechi kwa kitendo cha kumkanyaga Hazard.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt