asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Wednesday, April 5, 2017

PAMOJA NA MISUKOSUKO YA MADAWA YA KULEVYA......MAKONDA AZIDI KUWACHOKONOA VIGOGO WA SERIKALI....AJA NA HII MPYA KUHUSU MAFISADI


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amefunguka kuzungumzia namna ambavyo baadhi ya watu walivyotaka kupiga Tsh Bilioni 7 za serikali kwa kutaka kuwalipa watu hewa fidia za kupisha maeneo yao kwajili ya maendeleo ya miradi mbalimbali ya serikali.

Aidha RC Makonda ameiagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua watu ambao wamehusika katika sakata hilo.

Akiongea na waandishi wa habari Jumanne hii ofisini kwake jijini Dar es salaam, RC Makonda amesema amepewa jukumu na Rais Magufuli la kusimamia hela ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali kwajili ya maendeleo ya miradi mbalimbali ndani ya mkoa wa Dar es salaam.

“Mh Rais kama alivyoagiza na kuelekeza kwamba kila pesa inayotoka itoke kulingana na malipo halali. Mimi kama mkuu wa mkoa ninayo majukumu mengi ambapo moja wapo ni kusaini vitabu vya wananchi ambao wanakwenda kulipwa fidia katika maeneo mbalimbali ambako miradi inapita. 

Katika miradi ya DMDP ambayo inahusika na barabara, ujenzi wa mifereji na uboreshaji mji wa Dar es salaam. Katika vitabu ambavyo nilitakiwa kusaini kwajili ya kupitisha hizo fedha zaidi ya tsh biloni 10 vilikuwa vitabu 31, lakini katika uchunguzi wangu na team yangu nikagundua vitabu 8 zimekiuka taratibu mbalimbali na masharti, na watu hao hawastahili kulipwa, na katika bilioni kumi tumebaini zaidi ya bilioni 5 na milioni 700 ni fedha ambazo zilikuwa zinaenda kulipwa kwa watu hewa,” alisema RC Makonda.

Alisema katika wilaya Kinondoni kati ya tsh bilioni 6 na tsh milioni 600, zaidi ya tsh bilioni 1 na tsh milioni 800 zilikuwa zinaenda kulipwa kwa watu wasiostahili.

RC Makonda amedai katika jambo ambalo lilimshangaza kampuni ya mafuta ilipewa kazi ya kuthamini majengo na ardhi jambo ambalo lipo kinyume na taratibu.

Alisema katika taarifa ambapo alipewa aligundua kuna mtu alitakiwa kulipwa tsh milioni 4 kwajili ya shimo lake la taka


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt