asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Tuesday, May 2, 2017

MECHI YA SIMBA NA AZAM YAINGIA DOSARI....TFF YAINGILIA KATI USHIRIKINA ULIOFANYWA NA SIMBA...HAYA HAPA MAAMUZI YALIYOFANYWA...


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema linaendelea na uchunguzi kuhusiana na lile tukio la kishirikina lililofanywa na mwanachama wa Simba.

Mwanachama wa Simba aitwaye Ngade Ngalambe, aliingia na kumwaga kimiminika ambacho baadaye kilielezwa kuwa ni mafuta ya nguruwe.

Alifanya hivyo muda mchache kabla Simba haijaivaa Azam FC katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho na Simba ilishinda kwa bao 1-0.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema bado wanachunguza na baada ya hapo watachukua hatua.

“Tunaendelea kulifanyia uchunguzi suala hilo na endapo itabainika basi kanuni zipo wazi, hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya Simba na aliyefanya kitendo hicho,” alisema Alfred.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt