asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Wednesday, June 14, 2017

MCHEPUKO WA ZARI WAMREJESHA DIAMOND KWA SEPETU,..!!! DIAMOND AJA NA KUFUNGUKA HAYA

Diamond na Wema Sepetu
Mwanamuziki Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa yeye na aliyekuwa mpenzi wake, mrembo Wema Sepetu huwasiliana mara kwa mara na mara kadhaa hukutana kwa siri sehemu ambazo hazina waandishi wa habari au watu wengi.

Akizungumza leo katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Diamond Platnumz amemwagia sifa mrembo huyo na kusema kuwa amekuwa msaada mkubwa sana kwake hata wakati anaandaa manukato yake ya Chibu (Chibu Perfume).

“Mimi na Wema Sepetu huwa tunawasiliana kwenye simu, na mara kadhaa hukutana sehemu ambazo hazina watu wengi, kwa sasa tumekua. Kila mmoja wetu kwa sasa anajikita kwenye uhusiano wake. Wema Sepetu ana familia yake, lakini uhusiano wetu umejikita katika kusaidiana kibiashara.”

Diamond Platnumz aliongeza kuwa, Wema Sepetu ndiye aliyemshauri kutumia maneno “The Scent You Deserve” kwenye manukato yake aliyoyatambulisha hivi karibuni.

Diamond Platnumz na Wema Sepetu walikuwa ni ‘couple’ iliyowavutia wengi Afrika Mashariki lakini waliachana Novemba 2014 baada ya kuwepo tuhuma za kuchepuka kutoka kila upande.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt