Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inahitaji ushirikiano mkubwa na
wafanyabiashara, hivyo haitakubaliana na mtumishi yeyote wa umma
atakayefanya urasimu kwa lengo la kukwamisha uboreshaji wa sekta
binafsi.
Amesema
miongoni mwa maboresho yanayofanywa na Serikali katika sekta binafsi ni
pamoja na kuimarisha utendaji wa watumishi na kuondoa urasimu katika
utendajikazi wa kila siku baada ya eneo hilo limelalamikiwa sana.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Desemba 2, 2016) wakati
akizungumza na wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda mkoani Arusha kwenye
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) akiwa katika siku ya
kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Arusha.
Ziara
hiyo inalenga kuangalia utelelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya
CCM,Utendaji wa Serikali, kusikiliza na kujionea kero zinazowakabili
wananchi wa Mkoa huo na kushirikiana na viongozi wa Mkoa ili kuweza
kuzipatia suluhisho.
No comments:
Post a Comment