Amesema vikao hivo, “ni vitamu zaidi kuliko vile ya nje.”
Hayo
aliyasema Dar es Salaam alipofungua mafunzo ya siku mbili kwa
madiwani, wabunge na viongozi wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam
yanayoendelea kutolewa na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la
Ujerumani.
Akizungumzia
ziara za kanda zilizofanywa na viongozi wa chama hicho hivi karibuni,
Lowassa alisema vikao vya ndani vimewapa nafasi na muda mwingi wa
kuzungumza na wanachama kwa karibu zaidi.
“Tumefanya
ziara, tumeona hali ya barabara ni nzuri lakini hali ni nzuri zaidi
tulivyozungumza na wanachama wetu na tunamshukuru Rais.
“Aliona hakuna haja ya mikutano ya nje akatupatia vikao vya ndani, Loh! Ni vizuri, ni vitamu zaidi kuliko vile vya nje.
“Tunapata nafasi nzuri ya kuzungumza na wanachama ana kwa ana, kwa muda mrefu kwa mapenzi na mahaba.
“Nataka
niwaambie Chadema ipo imara sana. Watu walidhani wamekata tamaa lakini
wapo imara katika kuhakikisha chama kinapata ushindi mwaka 2020,”alisema Lowassa.
Alisema yapo malalamiko madogo madogo likiwamo watu wengi kutaka uongozi wa chama.
Alipendekeza yawepo mabadiliko katika katiba ya nchi kuongeza nafasi za uongozi.
“Wana
malalamiko madogo madogo lakini mengi ni ya uongozi, kila mtu anataka
kuwa kiongozi hadi nikakumbuka kule Kenya walipobadilisha Katiba
wakaongeza nafasi za uongozi, magavana, mameya na nyingine ili
zipatikane nafasi za siasa za kuongoza na mimi nadhani tungepata muda
tufafanue katiba ili ziongezwe nafasi za uteuzi.
“Au mnaonaje?” Lowassa aliwauliza wajumbe ambao kwa pamoja waliitikia: “Ndiyoo”
Alisema kuna kila dalili ya Chadema kushinda uchaguzi wa 2020.
Aliwataka
viongozi wa chama hicho kushikamana na kuepuka maneno ya kuwagawa
akisisitiza kuwa bila mshikamano hawataweza kushinda uchaguzi ujao.
“Dalili zote zinaonyesha tutashinda lakini kama tutakuwa wamoja.
“Bila
umoja hatuwezi kushinda na CCM wanajua maana ya umoja ndiyo maana
wanasema umoja ni ushindi, hivyo maneno ya kutugawa tusiyakubali,
viongozi tushikamane,” alisema Lowassa.
Alitaja
mbinu nyingine ya ushindi kuwa ni kwenda vijijini kutoa elimu kwa
sababu utafiti unaonyesha kuwa CCM imekuwa ikishinda maeneo yaliyo nyuma
katika elimu.
“Wakati
tukiwa Dodoma kwenye ziara kuna vijiji mtu anakuambia mimi nampigia
kura Nyerere (Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere), na akiona polisi
anakimbia.
“Sasa kama mtu anakimbia akimwona polisi anawezaje kulinda kura? Hivyo bila kwenda kutoa elimu vijijini hatuwezi kushinda,” alisisitiza Lowassa na kuongeza:
“
‘There is no time left’ (Hatuna muda wa kupoteza), muda uliobaki ni
mdogo sana hatuna budi kuutumia vizuri kwa kuangalia wapi tulikosea na
turekebishe vipi na tuongee kutoka moyoni tusiogopane.
“Tukosoane bila kusingiziana na tuone muda uliobaki tunafanya nini ili tushinde,” alisema Lowassa.
No comments:
Post a Comment