Kiongozi wa Gambia Yahya Jammeh amesema atakwenda mahakamani kupinga kushindwa kwake katika uchaguzi unaoweka kikomo cha utawala wake wa miaka 22.
Awali rais Rais Jammeh alikubali kushindwa baada ya mpinzani wake Adama Barrow kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa wiki iliyopita, lakini baadae alibadilisha kauli yake Ijumaa, akisema ''anakataa kwa ujumla'' matokeo.
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limemtaka akubali kushindwa.
Mitaa ya mji mkuu Banjul iko katika hali ya utulivu huku jeshi likipiga doria mjini humo.
Muungano wa Jammeh -Alliance for Patriotic Reorientation and Construction party Ulitangaza usiku wa Jumamosi , kwamba utawasilisha kesi katika mahakama kuu ya Gambia.
Kwa mujibu wa sheria za Gambia, malalamiko kuhusu matokeo yanaweza kupingwa kisheria katika kipindi cha siku 10 baada ya kupigwa kura.
Rais mteule Barrow Jumapili alisema kuwa anahofia usalama wake. Aliwahi kumshutumu Bwana Jammeh kwa kukiuka demokrasia kwa kukataa kukabidhi mamlaka.
Bwana Jammeh, ambaye alinyakua mamlaka kwa njia ya mapinduzi mwaka 1994, ameelezea kuweo kwa ''dosari'' katika upigaji kura na anataka uchaguzi urudiwe.
No comments:
Post a Comment