Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imekanusha uwepo wa taarifa juu ya ugonjwa wa ZIKA hapa nchini.
Waziri
wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake Dk. Hamisi Kigwangalla
wakitolea ufafanuzi jana mbele ya waandishi wa Habari, walisema wananchi
wasiogope na wamewatoa hofu kwani taarifa zilizotolewa awali na
kuripotiwa na vyombo vya habari walizonukuu kutoka NIMR hazina ukweli
wowote na ni za kupuuzwa.
Aidha,
kwa mujibu wa Kaimu Mkuu kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Afya), Bi.
Catherine Sungura katika taarifa ya Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu
ilieleza: “Napenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizoenea kwenye
vyombo vya habari na mitandao ya jamii kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Zika
nchini.
"Kama
nilivyoeleza mnamo tarehe 31 Januari 2016, ugonjwa huu bado haujaingia
nchini, na leo pia napenda kuwatoa hofu wananchi kuwa kwa sasa Tanzania
haujathibitishwa kuwepo na ugonjwa wa Zika. Utafiti uliofanywa na NIMR,
ulikuwa ni utafiti uliofanyika nchini wa kuchunguza ubora wa kipimo
kipya cha kupima magonjwa ya zika na chikungunya.
Kwa
utaratibu wa kitafiti, hii ni hatua ya awali tu ya kuangalia ubora na
uwezo wa kipimo hicho.Matokeo haya bado yanahitaji kuchunguzwa kwa kina
zaidi kupitia vipimo vilivyothibitishwa na Shirika la Afya Duniani.
Wizara
itaendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali mbali ndani na nje ya
nchi kuendelea na utafiti na ufuatiliaji wa kitaalamu ili kuzuia ugonjwa
huu kuwepo Tanzania.
Ufuatiliaji
wa magonjwa ni endelevu katika sekta ya afya na tuna taratibu za utoaji
taarifa wa magonjwa ya kuambukiza na hatari kama vile zika, ebola na
mengineyo.
No comments:
Post a Comment