Lori
la mafuta limelipuka nje ya mji wa Nivasha nchini Kenya usiku wa
Jumamosi December 10 2016 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.
Taarifa
iliyotolewa mapema leo December 11 2016 asubuhi na msemaji wa idara ya
taifa ya mambo ya dharura nchini Kenya Pius Masai amethibitisha kutokea
kwa vifo hivyo na kwamba magari zaidi ya 11 yameteketezwa kwa moto
katika barabara ya Nairobi-Naivasha.
Maafisa
kutoka wizara ya usafirishaji wakiongozwa na Katibu mkuu wa wizara hiyo
Irungu Nyakera wamewasili katika eneo la tukio na Taarifa zaidi
zinaeleza kuwa watu wengi wamejeruhiwa na miongoni mwao ni watu
waliokuwa wakirejea nyumbani kutoka harusini subukia.
Katibu
mkuu Irungu amesema kuwa kwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa ajali
hiyo imetokana na dereva kutokufahamu vizuri barabara hiyo kutokana na
kwamba lori hilo la mafuta ni la nchini Uganda.
No comments:
Post a Comment