Viongozi
wa Afrika Magharibi wamempa Yahya Jammeh nafasi ya mwisho kuachia
madaraka wakati majeshi ya Senegal yakiingia nchini Gambia tayari kwa
kumng’oa.
Jammeh
amepewa hadi Ijumaa hii mchana awe ameshachukua virago vyake ama
kuondolewa kwa nguvu na majeshi ya Afrika Magharibi yanayoungwa mkono na
Umoja wa Mataifa.
Jumuiya
ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, Ecowas inamuunga mkono Adama
Barrow, aliyeapishwa kama rais mpya wa Gambia, Alhamis hii katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal.
Ni
rais halali sababu ndiye alishinda uchaguzi wa mwezi uliopita na
amekuwa akitambulika kimataifa. Barrow, ambaye bado yupo nchini Senegal,
amedai kuwa hatarejea kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Banjul, hadi pale
operesheni ya kijeshi itakapokamilika
No comments:
Post a Comment