asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Saturday, December 17, 2016

Ndalichako awapa mtego Walimu wa masomo ya Sayansi



Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema walimu wa Sayansi watakaoajiriwa na serikali, watalazimika kutuma vyeti vyao kabla ya kupangiwa kituo cha kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Profesa Ndalichako, wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa wakuu wa shule za sekondari Tanzania (Tahossa). Pamoja na kuzungumzia mabadiliko hayo katika mfumo wa ajira, alisema nia ya serikali kuimarisha elimu ya sekondari, ikiwa ni pamoja na kuimarisha ufundishaji wa masomo hayo ya Sayansi.
Aidha alisema walimu wakuu wana wajibu wa kuwa wasimamizi na wakaguzi wa kwanza wa wanafunzi ili kuiboresha elimu ya Tanzania, wakizingatia kuwa elimu ya sekondari ni kiungo muhimu katika kuendeleza elimu nchini.
Vile vile, aliwataka wakuu hao kupeleka takwimu sahihi za wanafunzi waliopo katika shule zao ili kuisaidia serikali katika kupanga bajeti ili iweze kutoa fedha sahihi.
“Hapa kuna kimbembe wakati mwingine huwa najifanyisha nimepoteza takwimu ya shule fulani nikitumiwa inakuwa tofauti na ile ya mwanzo, niwaombe walimu mkalisimamie hili ili iwe rahisi kwetu kupanga bajeti yenye tija,” alisema.
Kwa upande wake Rais wa Tahossa, Bonus Nyimbo wakati akisoma risala aliiomba serikali itoe waraka wa kupiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi shuleni, kwani imekuwa ikichangia kushusha ufaulu wa baadhi ya wanafunzi


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt