asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Thursday, February 23, 2017

Sahau kuhusu Messi, hivi ndivyo Jordi Mboulo alivyowafanya watoto wa Dortmund kwenye Uefa (Video)

Wakati ukiwa unamfahamu Lionel Messi wa kikosi cha timu ya wakubwa ya Barcelona hutakiwi kusahau kwenye klabu hiyo katika timu yao ya vijana chini ya umri wa miaka 19 kuna kinda anaitwa Jordi Mboula ambaye anadaiwa kuwa Messi mpya katika timu hiyo.
Wakati timu hiyo ya wakubwa ikiwa na mlima mrefu wa kuupanda katika michuano ya kombe la mabingwa barani Ulaya baada ya kufungwa magoli 4-0 na PSG wiki iliyopita, Mboula Jumatano hii alifanikiwa kuiongoza timu ya vijana ya Barcelona katika mashindano kama hayo lakini ya vijana kuifunga Borussia Dortmund 4-1 wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani.
Mboula ambaye ana miaka 17 amezaliwa Hispania lakini pia ni raia wa Congo DRC alifanikiwa kufunga goli moja kati ya hayo manne lakini kubwa zaidi watu wameanza kumfananisha na Messi kutokana na alivyoonyesha uwezo wake mkubwa mpaka kupatikana kwa goli hilo



No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt