asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Thursday, February 23, 2017

WEMA SEPETU AFUNGA VIRAGO CCM AAMUA KUHAMIA CHADEMA


Mrembo Wema Sepetu Ameamua Kukikimbia Chama cha CCM baada ya Mh Paul Makonda Kumjumuisha katika watu wanaohusika na Madawa ya Kulevya na kufikishwa mahakani..

Picha kadhaa zimewekwa mtandaoni zikionyesha Wema Sepetu akiwa na Viongozi wa Chadema Akiwepo Muheshimiwa Mbowe....


Chama cha Demokrasia na Maendeleo kunatarajia kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo na chama hicho akiwamo msanii maarufu nchini wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu (28).


Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilianio wa Chadema, Tumaini Makene  amesema leo (Alhamisi) kuwa chama hicho kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia waandishi wa habari kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo Wema Sepetu.

Wema pamoja mama yake, leo aliongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa chama hicho kwenye mahakama kuu jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo aliyeshinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, alikuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuhamia Chadema.

Nini Maoni yako?
USIKOSE PIA HABARI HII....


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt