asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Tuesday, April 25, 2017

Jaji Lubuva Yamemfika shingoni!!!.....Aamua kuvujisha siri nzito ya uchaguzi 2015 iliyozua utata....Afunguka haya....!!!


Image result for jaji lubuva
WENYEKITI Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva amefichua mambo mbalimbali aliyokumbana nayo katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. 




Jaji mstaafu Lubuva, aliteuliwa kushika wadhifa huo mwaka 2011 na kustaafu Disemba mwaka jana na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage, amebainisha kuwa uchaguzi huo wa mwaka 2015 hatousahau kutokana na kuwapo kwa ushindani mkubwa.
Alisema kutokana na ushindani huo wa kivyama, baada ya matokeo baadhi ya ndugu zake walimnunia kwa kudhani kuwa haki hakutendeka jambo ambalo halikuwa na ukweli.

“Hata watu wengine ambao ni ndugu zangu walinuna, waliona hawakutendewa haki, lakini ndio kura kwani kwa mujibu wa kura Magufuli ndio kashinda.

“Katika uchaguzi wowote kuna mawili kushinda na kushindwa, anayeshindwa mara nyingi hawezi kuzungumza vizuri juu ya uchaguzi. Ila niseme uchaguzi ule uliendeshwa kwa taratibu na kanuni za uchaguzi, si kweli kwamba kura ziliibwa, kwa sababu tuliendesha uchaguzi kwa uwazi. Kwa mara ya kwanza kura za rais ziliwekwa wazi kwani vituo vyote vilibandika matokeo, hivyo mpiga kura anajua mgombea wake amepata nini ndipo tunaletewa huku Dar es Salaam tunajumlisha na kutangaza.

“Pia mawakala wao wanakuwapo na wanajua mgombea wao amepata kiasi fulani, hivyo niseme kuwa hakuna sehemu jimbo wala wilaya kwamba kura za mgombea urais ambazo zilitangazwa makao makuu hapa Dar es Salaam ambazo zilikuwa batili. Hivyo unaposema kura zimeibiwa ushahidi upo wapi? Ndio hicho ninachozungumza wakati wote kuwa kadiri matokeo yanapokuja ndivyo nilivyokuwa nayasoma,” alisema.
Aidha, Jaji Lubuva alisema licha ya kuwapo baadhi ya kundi la vijana waliomtishia kumuua iwapo kungetokea matokeo wasiyoyataka, anamshukuru Mungu uchaguzi huo ulifanyika kwa amani bila vurugu na kamwe hakuwa na hofu.

“Sikuwa na hofu, tunajua baadhi ya vyama walikuwa na sehemu zao wanaita Ngome, walikuwa wamejiandaa sana kwamba labda kufanya fujo ila nilikuwa nimejiandaa vizuri kwani hata hivi vyama vya upinzani kwa ujumla walishirikiana na chama tawala baada ya matokeo. Kama kweli wangedhamiria kufanya fujo basi wangewachochea vijana wao, na kwa sababu sikufanya lolote baya ndani ya utendaji wangu hapakuwapo na uvunjifu wa amani. Kuna baadhi ya vijana walikuwa wanatishia kuniua iwapo ningetangaza matokeo tofauti na walivyokuwa wakitaka lakini bahati nzuri hapakuwapo na lolote uchaguzi uliisha kwa amani,” alisema
Licha ya baadhi ya Watanzania kudai kuwa NEC si huru, Jaji Lubuva alisisitiza kuwa Tume hiyo ni huru kwani hata katika kipindi cha uongozi wake hapakuwahi kutokea wito wa Rais kuwataka viongozi hao wafike Ikulu.

“Nimelizungumza sana tangu nimeingia pale, kwamba yapo madai kwamba Tume si huru, nimesema kwamba hizi ni hisia kwamba Jaji Lubuva ni mteule wa rais na mkurugenzi na makamishna ni wateule wa rais, pia wakati rais huyohuyo ni mwenyekiti wa chama. Lakini siku zote nilisema tume inafanya kazi zake kwa uhuru, hakuna siku yoyote tumeingiliwa na rais na hata sasa nimeicha NEC ikiwa huru. “Kwa sababu tumekuwa tukishirikiana na tume za nchi za EAC na SADC baadhi yao wanajiita tume huru, ila sisi hatukujiita jina hilo ila niwahakikishie kuwa tume yetu ni huru kabisa.

“Kama mtakumbuka Tume ilikwenda kwa Jaji Warioba kipindi cha kuandaa rasimu ya Katiba, tukawasisitizia kuwa tunafanya kazi kwa uhuru ila kuondoa hayo maono ni vyema kuangalia namna ya kubadilisha kidogo vifungu vya sheria. Kwa sababu pamoja na rais kuteua makamishna, mkurugenzi na hata Jaji mkuu hapakuwapo kabisa na mwingiliano wowote, tangu niwapo pale hata siku moja hatukuwahi kuitwa na rais Ikulu,” alisema


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt