asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Tuesday, April 25, 2017

MAKONDA AITIA DOSARI BONGO MOVIE.... AWANASA JB NA WEMA SEPETU KATIKA MTEGO HUU...!!!




Muigizaji mkongwe nchini Jacob Stephen 'JB amefunguka na kudai hawakufanya maandamano ya kuzuia movie za nje ya nchi kuuzwa nchini bali waliandamana kuzitaka zilipiwe kodi au serikali itoe msamaha kwenye filamu za ndani.

JB amezungumza hayo alipokuwa akifanya mahojiano na wanahabari wakati wa uzinduzi wa filamu ya Tunu na kudai kuwa watu wengi wamehusisha maandamano yao na Makonda na siasa kitu ambacho hakina ukweli na kuongeza kuwa tasnia ya filamu kwa sasa inahitaji watu watakaowasaidia kumaliza kilio chao. "Sisi hatupingi movie za nje kuingia nchini, mimi mwenyewe nazipenda na ninaziangalia. Hapa ugomvi uliopo ni wao watozwe kodi au na sisi tuondolewe hizo kodi, wakifanya hivyo hakuna mtu ambaye atapiga kelele tena. Sasa hivi nakatwa asilimia 30 lakini bado natakiwa nitoe asilimia tano na wakati huo huo, nikitaka kutoa movie mpaka nikaombe kibali kama ni wewe ungekubali? Na jambo hili lisihusishwe na siasa kwani sisi mtu yoyote ambaye ataweza kutusaidia kutusemea tutamsikiliza hata akiwa wa upinzani hatuna shida" Alisema Jb

Aidha msanii huyo ameongeza kuwa wasanii wenzao wanaowakejeli kwa kuandamana akiwemo Sepetu wengi wao hawategemei movie kuwaingizia kipato na ndio maana wanaongea maneno ya ajabu huko nje. "Msanii yoyote ambaye filamu ndiyo chakula chake hawezi kuwa nje ya hili kwa sababu hataweza kuishi. Mimi niseme tu siwezi kuishi bila filamu ndiyo maana tunapiga kelele. Sitaki kuwataja majina lakini angalia tu wewe mwenyewe huyo mtu ambaye hataki kupiga kelele anaishi bila filamu?" JB alimaliza


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt