Meya
wa Manispaa ya Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo
(CHADEMA), Boniface Jacob amemtaka Rais Dk Magufuli kulichukuwa shamba
linalomilikiwa na Rais Mstafuu Mzee Benjamin Mkapa kama alivyofanya kwa
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Meya
huyo alisema kuwa kiongozi huyo wa zamani na familia yake wanamiliki
shamba kubwa katika wilaya ya Ubungo ambalo halijaendelezwa kwa muda
mrefu sasa.
Meya
huyo ambaye amekuwa Diwani wa Ubungo kwa muda mrefu ametaa shamba hilo
lililopo Mbezi, Dar es Salaam lirejeshwe kwenye halmashauri ili liweze
kufanyiwa shughuli nyingine.
Hoja
hiyo ya Meya wa Kinondoni imekuja siku chache tangu aliyekuwa Waziri
Mkuu katika serikali ya awamu ya tatu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya
CHADEMA, Frederick Sumaye aliponyang’anywa shamba lake eneo la
Mabwepande ambalo hajaliendeleza kwa muda.
Meya
alitoa maelezo hayo alipokuwa akizungumza na gazeti la mwananchi ambapo
alisema kuwa watamuandikia Rais Magufuli barua wakimuomba abatilishe
umiliki wa shamba hilo aipe Manispaa ya Ubungo ambayo ndiyo kwanza
imeanzishwa.
No comments:
Post a Comment