Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu
Hassan akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 70 na laki nne kwa
ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Chato kutoka kwa Balozi wa China
nchini Dkt. Lu Youqing wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za
maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu
Hassan akihutubia mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam leo wakati
hafla ya kufungua sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Jamhuri ya
watu wa China.China inasherehekea Mwaka Mpya ambapo mwaka huu umepewa
jina la Jogoo (Rooster).
Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Dkt. Lu Youqing akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa
China leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wakifuatilia mambo mbalimbali
yaliyokuwa yakiendelea katika hafla ya kuadhimisha mwaka mpya wa China
leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wakitembelea baadhi ya mabanda
yaliyopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
yam waka mpya wa China leo jijini Dar es Salaam. China wanasherehekea
mwaka mpya leo na kesho katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 4:00
asubuhi hadi saa 11 jioni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu
Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya
Tanzania na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing baada ya
kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya
wa China leo jijini Dar es Salaam.Maadhimisho hayo yanafanyika katika
viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 4;00 asubuhi hadi saa 11 jioni na
yanatarajiwa kumalizika kesho tarehe 22 Januari 2017.
No comments:
Post a Comment