Siri iko kwenye kifungua kinywa!
Kibongobongo tunaita chai, ila kwa Kiswahili sanifu ni kifungua kinywa. Hiki wataalam wanasema kazi yake si kufungua kinywa tu, hata ubongo unafunguka. Tafiti zinaonyesha kuwa watoto wanaopata kifungua kinywa wanafanya vizuri kwenye test za kuangalia attention na kumbukumbu, kuliko wale wasiopata kifungua kinywa. Na wote tunajua, attention darasani ndio inamfanya mtoto aelewe, afu kumbukumbu ndio inamfanya afanye vizuri kwenye mtihani au hata application ya vitu alivyojifunza baadae. So bila hivyo vitu viwili mtoto kufanya vizuri darasani si rahisi.
Kwa nini chai/kifungua kinywa?
Kwa sababu chakula ndio mafuta ya miili yetu, sasa mtoto anamka mafuta yamepungua, inabidi ajaze tank lake (tumbo) ili kila kitu kiende sawa, including brain yake.
Ila sio kila chakula kina the same effect. Lakini kitu chochote ni better than nothing, maana watoto wengine wanachagua sana vyakula.
Baadhi ya vyakula vya kurutubisha ubongo:
- Peanut butter (siku hizi ziko kibao, mini market yeyote unapata)
- Mayai
- Ndizi mbivu
- Maziwa
- Mtindi
- Asali (unaweza kuipaka kwenye mkate)
No comments:
Post a Comment